HTML Tables
Burudani

DR KIGWANGALLA AMPA TANO RAY C

Dr Kigwangalla

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hamisi Kigwangalla, amesema amefurahishwa na kuvutiwa sana na jitihada za kuimba anazofanya Rehema Chalamila (Ray C) huku akiomba Wantanzania kumuunga mkono msanii huyo.

Dr Kigwangalla, ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe unaomuhusu msanii huyo kama hivi:

Na Mimi kama Naibu Waziri wa Mambo ya Wanawake, kama #BaloziWaWanawake na kama Daktari niseme nimefurahishwa na kuvutiwa sana na jitihada anazofanya huyu dada @rayctanzania, nimeguswa na wimbo wake wa #Unanimaliza, na nimeona nimuunge mkono kwa kuwaomba wadau wote ambao mmekuwa naye siku zote mfahamu kuwa sasa anahitaji support yetu zaidi kuliko wakati wowote ule. Tumuunge mkono kwa dhati. Mungu atatujaalia kheir kwenye maisha yetu pia. Hakuna aliyekamilika. Sote tuna vipindi vyetu vya kuanguka Na kwa hakika tunahitaji ‘a second chance’ kila siku za maisha yetu! Hakuna anayeweza kujisimamia mwenyewe, sote tunahitaji mtu mmoja wa kutushika mkono na kutunyanyua pindi tunapoanguka! Kila la kheir Ndg. Rehema Chalamila. With our support, even the sky is not the limit! Keep on moving, keep on believing! #TeamBelieve #NjeYaBox #TanzaniaTuitakayo #MzeeWaField #SiasaNiVitendo #BaloziWaWanawake

Kwa upande wake Ray C nae amemjibu Dr Kigwangalla hivi:

” Heshima kwako Muheshimiwa, Nashukuru sana kwa maneno yako ya faraja baba. Bless your soul Sir.”

24,Machi mwaka huu, Dr Kigwangalla alimsifia Diamond Platnumz kuwa ni mjasiriamali mzuri baada ya kuzindua Chibu Perfume.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top