HTML Tables
Burudani

DOGO JANJA: MUZIKI NINAOFANYA MIMI NI LEVEL NYINGINE.

Msanii kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja amejitamba na kusema ingawa yeye ni mdogo lakini muziki anaofanya ni mkubwa kiasi kwamba watu wanaoweza kuufanya ni level za Jay Z

Msanii huyo  amesema kwanza yeye si mtu wa kushirikishwa au kushirisha wasanii hovyo hovyo katika nyimbo zake, bali yeye anadeal na zile serious project tu.

“Mtoto anafanya muziki wa mtu mzima, muziki ninaofanya mimi angetakiwa afanye mtu kama Jay Z lakini ndio nafanya mimi, ni hatari sana,” amesema na kuongeza.

“Mimi kwanza sifanyi kolabo, kama nitafanya ni zile zipo serious, sio zile kuna kaverse kapo hapa njo ufanye, kama unafiti ibuka. Mimi nafanya project kama ya Chindo ametoka Marekani straight L. A (Los Angeles), mimi nikatoka straight froma Dar es Salaam tukakutana Arusha tukashoot video Kijenge, madirector wanne kutoka nje, tumemaliza mimi nikasepa kuendelea na mitikasi mwana akala flight to L.A,” amemaliza kwa kusema.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top