HTML Tables
Burudani

DAZ AFUNGUKA MCHAWI WAKE

Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop, Daz Baba amedai amegundua kitu ambacho kinamkwamisha ashindwe kufanya vizuri kama zamani

Daz ambaye amewahi kufanya vizuri na nyimbo nyingi ikiwemo ‘Namba 8’, amesema kuwa uwekezaji katika kazi zake za muziki ndio kitu ambacho kinamfelisha.

“Mimi kitu ambacho kinanikwamisha kwa sasa ni video kali. Kwa sababu nyimbo zangu ni kali sana na sijawahi kufanya kazi mbaya katika maisha yangu,” alisema Daz. “Kama ningepata management kali ya kusimamia muziki wangu na kuwekeza ningerudi vizuri kwenye game,”

Aliongeza, “Siwezi kukata tamaa na bado napambana najua bado nafasi ya kufanya vizuri ninayo kwa sababu kila kitu ninacho katika muziki wangu,”

Daz Baba

Daz amedai kwa sasa anatafuta management ambayo itasimamia muziki wake.

Rapa huyo ni mmoja kati ya wasanii wa Kundi la Daz Nunda ambao walifanya vizuri katika kipindi cha nyuma.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top