HTML Tables
Habari

DARAJA LA KIVULE LASOMBWA NA MVUA

Daraja la Kivule limesombwa tena na mvua ya jana Jumatano jioni na kusababisha adha kubwa kwa wananchi.

Hii ni mara ya pili kwa daraja hilo kukatika ndani ya wiki hii kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, Kutokana na tatizo hilo vijana wamebuni mradi wa kuvusha watu kwa sh 500 na pikipiki kwa Sh 2,000.

Mmoja wa vijana hao, Festo Songoro amesema ameanza kazi hiyo tangu alfajiri na hadi saa 2:00 alikuwa amevusha zaidi ya watu 20.

Diwani wa Kata ya Kivule, Wilson Mollel amesimamia matengenezo ya kivuko cha miguu na watu wameanza kuvuka saa 2:30, Amesema amewasiliana na mkandarasi anayejenga daraja hilo ili kutafuta suluhusho la kudumu.

1 Comment

1 Comment

  1. Khadija Abdallah

    Khadija Abdallah

    March 9, 2018 at 11:58 am

    Jamani xelikali

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top