HTML Tables
Habari

BOCCO ,MBONDE KUIKOSA YANGA, OMOG BADO YUPO SANA SIMBA..

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano Haji Manara leo amekutana na waandishi wa habari ambapo ameelezea juu ya hali ya wachezaji ambao kwa sasa ni majeruhi hususani John Bocco pamoja na Salim Mbonde ambao wamepata majeraha katika mechi iliyopita dhidi ya Mtibwa Sugar.

 

 

 

John Bocco ameshafanyiwa vipimo ambapo kutokana na ushauri wa daktari ataukosa mchezo dhidi ya Njombe FC huku Salim Mbonde majeraha makubwa aliyoyapata kwenye goti yana mpelekea sasa kukaa nje na kukosa mechi nne mfululizo dhidi ya Njombe FC, Yanga, Mbeya City pamoja na Tanzania Prisons.

 

 

 

Kuhusina na Nduda pamoja na Kapombe, mkuu wa kitengo cha Habari Haji Manara alieleza kuwa Nduda amesharejea Tanzania kutokea nchini India kwa matibabu ambapo baada ya matibabu yale atakuwa nje kwa muda wa wiki 8, Kapombe bado madaktari wameendelea kushauri aendelee kukaa nje chini ya uangalizi wa Daktari mpaka pale atakapopona kabisa.

 

 

 

Pamoja na taarifa hiyo Haji Manara aliendelea kukanusha uvumi mbaya unaoenezwa kuhusiana na kocha Omog, kuwa uongozi wa Klabu ya Simba bado upona imani kubwa na kocha Omog akisaidiana na kocha Jackson Mayanja.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top