HTML Tables
Michezo

BARCELONA MABINGWA LA LIGA

Lionel Messi akishangilia baada ya kuifungia Barcelona mabao matatu peke yake dakika za 38, 82 na 85 katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Deportivo La Coruna kwenye mchezo wa La Liga usiku wa Jumapili Uwanja wa Manispaa ya Riazor. Bao la kwanza la Barca ambayo kwa ushindi huo inajihakikishia taji la 25 la La Liga lilifungwa na Philippe Coutinho dakika ya saba, wakati mabao ya Deportivo La Coruna yamefungwa na Lucas Perez dakika ya 40 na Emre Colak dakika ya 64

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top