HTML Tables
Michezo

AZAM FC WAPANIA KUFANYA MAAJABU LEO HUKO MBEYA

Msimu uliopita Azam FC, ilifanya maajabu kwa kujiandikia historia baada ya kupata pointi tatu kwa mara ya kwanza dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.
Azam FC itaingia tena ndani ya uwanja huo kesho Jumapili kusaka ushindi dhidi yamaafande hao wa magereza, na kuendeleza rekodi hiyo kwa mara ya pili mfululizo kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Kikosi hicho kinachodhaminiwa na Maji safi ya Uhai Drinking Water, Benki ya NMB na Tradegents, kipo vizuri kabisa kuelekea mchezo huo na wachezaji wana morali ya hali ya juu ya kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

Azam FC itaingia dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Majimaji kwenye mchezo uliopita huku Prisons wakitoka kuifunga Mbeya City mabao 3-2 katika mchezo wa mahasimu wa jiji la Mbeya ‘Mbeya Derby’.
Akizungumza kuelekea mtanange huo muhimu kabisa kwa matajiri hao viunga vya Azam Complex katika kampeni yake ya mbio za ubingwa, Kocha Mkuu Aristica Cioaba, alisema kuwa wanaingia kwenye mchezo huo kwa kazi moja tu ya kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

Click to comment

You must be logged in to post a comment Login

Leave a Reply

To Top